ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, July 3, 2010

OH AFRICA!!!!!

ITACHUKUWA MIAKA AFRIKA KUUGUZA DONDA HILI.

Heartbroken Ghana star Asamoah Gyan received a message of condolence from Nelson Mandela after his devastating penalty miss led to his team’s dramatic World Cup exit against Uruguay.

Former South African president Mandela, who sent a letter of support to the Ghana team before the match, was further moved to pass on his sympathy to Gyan upon seeing the forward in a flood of tears after missing a chance at winning a place in the semifinal.Ghana took the lead just before halftime thanks to a brilliant long-range strike from Sulley Muntari, but was pegged back when Diego Forlan smashed home a superb free kick after the break.

ANGUKO LA SOKA AFRIKA.

“This is cruel,” Ghana coach Milovan Rajevac said. “But it is football. What can you say to him [Gyan]? We were so close and somehow it did not happen. We were so close to history.

“There were times when it seemed like there was someone else in control of this, someone above.”

With host nation South Africa having been dumped out of the tournament early on, local sentiment switched heavily to Ghana, which enjoyed huge crowd support.

But on a night that twisted and turned with reckless frequency, it was not enough.

Friday, July 2, 2010

SHEREHE KABLA YA SHEREHE ZAWAPONZA BRAZIL.

GOLI LA BRAZIL MFUNGAJI AKIWA KAKA, KABLA YA KIBAO KUWAGEUKIA.

PORT ELIZABETH, July 2 (Reuters) - Wesley Sneijder ndiye aliye inyanyua toka nyuma timu ya uholanzi hatimaye kuwatandika wanaume kumi wa Brazi 2-1 hivyo kukata tiketi ya kuingia nusu fainali kombe la dunia.

Brazil, mabingwa mara tano wa kombe hilo, iliwachukuwa dk kumi kuongoza kupitia goli la mfungaji wao mahiri Robinho nakumiliki mchezo kipindi chote cha kwanza dhidi ya Wadutch hao.

PRODUCER Q. WA MO RECORDS KUOA JUMAPILI HII.

YULE PRODUCER MAHIRI WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA HAPA BONGO ALIYEGONGA PINI KAMA 'WE NDO MCHIZI WANGU' BY N2N NA NYINGINE KIBAO Q.THE DON, ANATARAJI KUFUNGA NDOA TAKATIFU KATIKA KANISA LA ANGLICAN NYAMANORO JIJINI MWANZA. KWA MUJIBU WA TAARIFA ZA KIKAO CHA MWISHO CHA HARUSI YAKE KILICHOFANYIKA JANA PK HOTEL JIJINI HAPA. NDOA HIYO ITAFUNGWA JUMAPILI HII TAREHE 4 JULY 2010. TAYARI NDOA HIYO IMETANGAZWA KANISANI IKIWA NI MARA YA TATU.
KILA LA KHERI BROOO.


CHIAZZZZ! NA TUFUNGE KIKAO KWA LEO.

MV NG'OMBE NI MALI, YATEKETEA WAKATI IKING'OA NANGA.

Moto umetokea jana majira ya saa 2 usiku na kudumu kwa zaidi ya masaa matatu umeiteketeza kabisa boti ya Mv Ng'ombe ni mali.

Boti hiyo inayofanya kazi zake za kusafirisha bidhaa mbalimbali kutoka na kuingia ktk visiwa vilivyopo ndani ya ziwa Victoria, ilikumbwa na dhahma hiyo wakati iking'oa nanga, chanzo kikitajwa kuwa ni shoti iliyotokea upande wa plug ktk injini ya boti hiyo, ile kuwasha tu! ikawa kama kibiriti kwa mapipa ya mafuta ya taa na petrol yaliyokuwemo kwenye chombo hicho

"Katoni 10 za tingisha, dumu 6 za maji ya breweries na box 20 za maji ya kilimanjaro" Mfanyabiashara Januar Mgalula akisimulia mali zake zilizoteketea. Zaidi ya mapipa 240 pamoja na bidhaa mbalimbali zilizokuwa zikisafirishwa kuelekea visiwa vya Bulubi na kisiwa cha Ghana zimeteketea ktk moto huo.

Wananchi wakishuhudia moto chini ya ulinzi wa kutowaruhusu kulikaribia eneo la tukio.

Kamanda wa polisi wilaya ya Ilemela mama Matola akichukua taarifa.

Boti ikiteketea.

Zimamoto katika tukio hili kama vile walikuwa darasani wakifanya majaribio.

Alhamdulilah! Vijana hawa waliokuwa wakisaka masalia asubuhi ya leo wameibuka na mfuko wa sukari uliokuwa chini kabisa.

WAMILIKI WA MALI ZILIZOKUWEMO KATIKA CHOMBO HICHO KILICHOTEKETEA.

HALI ASUBUHI YA LEO.
Mazingira haya tusinge yaona leo hivi kwani kuna baadhi ya boti zilizokuwa karibu na boti iliyoungua, zikisubiri safari siku inayofuata wamiliki wamiliki wake hawakuwepo eneo la tukio, msaada wa kukata kamba za nanga ulifanyika kuzinusuru. Kwani Kulikuwa na kila dalili ya moto huo kusambaa eneo zima na kuteketeza kila kilichopo pande hizo.

Thursday, July 1, 2010

TUSHAZOEA.

Kibonzo na NATHAN WA MAJIRA.

NIKAMA ANASEMA:-"OooH Vituo viongezwe! OooH Muda hautoshi!
Haya sasa muda umeongezwa, watu hola!Wasajili tunapigwa dolo.
Ule msongamano hapa kituoni sijui umekwenda wapi? Kwa mpango huu..
We ngaja tu! muda ukikaribia kwisha, wakija kwa wingi kusajili bila buku jero, sisajiri mtu"


SAKATA LA UWANJA HUU WA NYAMAGANA NI KAMA BOMU VILE LINALOSUBIRI MUDA WAKE KULIPUKA.

MAWIO HADI MACHWEO NI JADI KUONA MSONGAMANO HUU KATIKA ATM ZA BENKI YA NMB MWANZA, PPF TOWER.

BARABARA YA KENYATA TAWI JINGINE LIKIWA KWENYE UKARABATI.

EYO MCHOMVU!!! KAONA NINI?


MCHIZI KAMA ANASHANGAA VILE KUONA MPIRA WA JABULANI UNAO WAPONYOKA MAKIPA WAKAPIGWA BAO! AU VUVUZELA LINALOWAZINGUA WENYE MABUsher NA WADHUNGU WANAOKOMPLEIN KELELE!!!? AU PENGINE ILE FIRE EXTINGUISHER KULEEEEEeeee!!!!
AU PENGINE ANAMWAMBIA LOVENESS LOVE “NIMEONA KAKITU HAPOOO, JIPANGUSEEEEE!


BRAAAAh! BRAAAAh!
KICHWA IMEJAA MAJIBU NA MASWALI YAKUMWAGA.
MSAADA KWENYE TUTAZ!

WAKONGO WAISHIO UINGEREZA WAZINDUA KAMPENI KUSAIDIA WATU WENYE MARADHI.

RAIS JOSEPH KABILA NA MFALME ALBERT WA BELGIUM SIKU YA KUADHIMISHA MIAKA 50 YA UHURU WA CONGO.

Jamii ya watu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaoishi nchini Uingereza wamezindua kampeni maalum mjini London, iitwayo Congo Unite.

Lengo ni kuchangisha fedha ili kuwasaidia watu wenye maradhi ya selimundu (sickle cell) na watoto walioachwa yatima kutokana na maafa ya vita nchini Congo.

Kampeni hiyo imeanza kwa uzinduzi wa mkanda maalum wa video na CD za wimbo maalum uitwao Congo Unite ulioimbwa kwa kuwashirikisha wasanii mbalimbali wa Congo wanaoishi nchini Uingereza.

Video hizo zitauzwa duniani kote kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia mpango huo.

Kampeni hii imepewa jina la Congo Unite ikiwa ni wito kwa raia wote wa Congo duniani kusahau tofauti zao na kuungana na kushirikiana kwa pamoja katika kujaribu kusaidia kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili raia nchini humo.

Kampeni hii imeanza kwa kulenga kuwasaidia watu wanaokabiliwa na ugonjwa wa selimundu, watoto yatima na matatizo mengine yatokanayo na maafa ya vita.

Akizungumza na BBC mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa CONGO50 ambaye pia ndiye aliyeongoza utengenezaji wa video hiyo ya Congo Unite amesema mbali na kutumia fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo ya CD na Video hizo kutumika kusaidia waathirika wa selimundu, wanategemea pia kuanzisha kituo cha kulelea watoto yatima nchini Congo.

Naye mratibu wa kampeni hiyo, Mimi Zabu Litambola, amesema moja ya mambo yanayotiliwa mkazo ni kukusanya fedha ili kutafsiri vitabu na maelezo kuhusu ugonjwa wa selimundu kutoka lugha ya kiingereza kwenda katika lugha zote zinazutumika nchini Congo.

Hatua hiyo itaiwezesha jamii ya Congo kupata elimu ya kutosha juu ya ugonjwa huo.

Kampeni ya Congo Unite ni moja ya mipango iliyoandaliwa na raia wa Congo nchini Uingereza katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wednesday, June 30, 2010

ASKARI WA RIVER CAMP NDANI YA PASSION FM.

MICHANO TIME 14:00 HADI 16:00.
MAJIRA YA MCHANA LEO NDANI YA PASSION FM KIPINDI CHA 'MICHANO TIME' KINACHOONGOZWA NA MTANGAZAJI WAKO MAHIRI FILBERT KABAGO NA KWENYE MOJA NA MBILI AKISIMAMA DJ GEORGE HUMO NDANI KILIVAMIWA NA ASKARI WA R' CHUGA, JOE MAKINI NA BONTA.


Joe makini:-"KWA WALE WANAO SEMA HIP HOP IS DEAD NI MATATIZO YAO BINAFSI, NAMAANISHA HIP HOP IMEKUFA KATIKA NAFSI ZAO, UTENDAJI, UPEO WA KUFIKIRI NA SI KWA MSANII KAMA JOE MAKINI, AMBAYE KWAKE 'HIP HOP IS ALIVE' KWANI KILA NINAPOPIGA SHOW WATU WANAFUNGUKA, WANAIMBA NAMI, MARAFIKI WANAPATANA, WENGINE WANADUMISHA MALOVEE' AT THE END NAFUNIKA. SO DON TEL ME THAT HIP HOP IS DEAD, IS DEAD ON YA SIDE NAT ME"

Bonta:-MIE NAUZA KURA YANGU TU! NA UKITAKA KUINUNUA FANANA NA KINONDONI, FANANA NA MWANZA MWANZA AU ARUSHA NI HAYO TU!

Joe makini:-ALBUM IMEKWISHA KAMILIKA YAITWA 'SIJUTII' NA SI MUDA MREFU ITAKUWA SOKONI, NILIPASHWA KUTOA 'DOUBLE ALBUM' LAKINI MARIDHIANO HAYARUHUSU MEY B' NEXT TIME ARIFF NITAFANYA HIVYO.

Kabago:-NINI USHAURI WAKO KWA WASANII WANAOCHIPUKIA WAFANYAO HIP HOP.

Joe Makini:-WANAPASWA KUZUNGUMZIA VITU VYA MSINGI VYA UKWELI VINAVYOTOKEA KATIKA JAMII NA ULIMWENGU KWA UJUMLA, KAMA NI UCHUMI, MAPENZI, SIASA AU NASAHA IWE REAL' ISIWE VITU VYA KUFIKIRIKA.
MWISHO NAWASHUKURU MASHABIKI NA MARAFIKI KWA SAPOTI KTK SHOW.

OPRAH WINFREY, ATISHA KWA UTAJIRI.

Mtangazaji wa televisheni Marekani Oprah Winfrey ametajwa kuwa mtu mwenye mvuto na utajiri mkubwa duniani kupitia jarida la Forbes.

Winfrey amempiku muigizaji wa filamu Angelina Jolie kwenye nafasi ya kwanza ya orodha ya watu 100 mashuhuri kwa mwaka katika jarida la Forbes.

Nafasi hizo hupangwa kutokana na mapato ya mtu na kiwango anachoonekana kwenye vyombo vya habari.

Muimbaji Beyonce, amechukua nafasi ya pili, huku mkurugenzi wa filamu James Cameron akiingia tena kwenye chati na kuchukua nafasi ya tatu kufuatia mafanikio yake ya filamu ya Avatar.

Lady Gaga amepanda katika nafasi mpya ya orodha hizo akiwa nafasi ya nne.

Kama ilivyo kwa Beyonce, mapato yake na taarifa za maisha yake kwa ufupi zimeongezeka katika miaka 12 iliyopita kutokana na ziara zake duniani na mikataba mbalimbali.

Jolie, wakati huo huo, ameteleza kutoka nafasi ya juu hadi kufikia nafasi ya 18.


Nyota wa gofu aliyezingirwa na matatizo mengi Tiger Woods ni nyota pekee wa michezo kuwa katika 10 bora.

Britney Spears amekuwa wa sita, ikufuatiwa na U2 kwenye nafasi ya saba, wakiwa wamerudi katika 100 bora.







SANDRA BULLOCK.
Sandra Bullock, aliyeshinda tuzo ya Oscar mwaka huu ya muigizaji bora wa kike, amepanda chati kwa kasi kutoka nafasi ya 92 hadi kufikia ya nane.

Johnny Depp naye amerudi kwenye chati katika nafasi ya tisa.

Kigogo wa muziki Simon Cowell ameongoza kwa upande wa Uingereza, kwa kupanda nafasi 14 hadi kufikia nambari 11.

Lakini Clodplay imeshuka kwa nafasi 20 na kuwa ya 35 katika mwaka ambao bendi hiyo imepumzika kufanya ziara na kuamua kurejea studio.

Nyota wa Harry Potter Daniel Radcliffe ameshika nafasi ya 82.

Umaarufu wa mfululizo wa Twilight ulionekana kwa kuwepo muigizaji wa kike Kirsten Stewart akiwa nafasi ya 66 na Robert Pattinson nafasi ya 50, wote wakiwa kwenye orodha hiyo kwa mara ya kwanza.

Mwaka huu, Forbes iliongeza kigezo cha mtu maarufu kuwepo kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook au Twitter, pamoja na mapato na kiwango cha kuonekana kupitia vyombo vya habari.

Britney Spears amekuwa wa sita, ikufuatiwa na U2 kwenye nafasi ya saba, wakiwa wamerudi katika 100 bora.

Sandra Bullock, aliyeshinda tuzo ya Oscar mwaka huu ya muigizaji bora wa kike, amepanda chati kwa kasi kutoka nafasi ya 92 hadi kufikia ya nane.

CHEKA KIDHUNGU!


A man comes to his doctor and tells him that his wife doesn't want to have sex with him for the last 7 months. The doc tells the man to bring his wife in so he can talk to her. So the wife comes into the doctor's office and the doctor asks her what's wrong and why doesn't she want to have sex with her husband any more.

The wife tells him, "For the last 7 months every morning I take a cab to work. I don't have any money so the cab driver asks me, 'So are you going to pay today or what?' so I take a 'or what'. When I get to work I'm late so the boss asks me, 'So are we going to write this down in the book or what?' so I take a 'or what'.

Back home again I take the cab and again I don't have any money so the cab driver asks me again, 'So are you going to pay this time or what?' so again I take a 'or what'. So you see doc when I get home I'm all tired out, and I don't want it any more."

The doctor thinks for a second and then turns to the wife and says, "So are we going to tell your husband or what?"

Tuesday, June 29, 2010

WAZIRI MKUU WA KENYA RAILA ODINGA AFANYIWA UPASUAJI.


Daktari wa Waziri Mkuu Raila Odinga, Oluoch Olunya, amethibitisha kuwa Odinga amefanyiwa upasuaji katika ubongo wake baada ya kubainika kuwa kulikuwepo na shinikizo kubwa katika kichwa chake.

Daktari Olunya aliyekuwa akihutubia waandishi wa habari kuhusiana na kulazwa kwa Waziri Mkuu katika hospitali ya Nairobi, amesema kwamba Waziri Mkuu aliwaambia kuwa aligonga kichwa chake kwenye gari lake majuma matatu yaliyopita.

Mtaalamu huyo wa upasuaji wa ubongo amesema kuwa Odinga anaendelea kupata nafuu na kwamba ameweza kukaa kwa urahisi katika chumba chake hospitalini.

Muuguzi huyo pia amesema Raila ana uchovu mwingi mwilini na anahitaji kulazwa kwa siku tano zijazo.

Awali taarifa kutoka kwa ofisi yake ilidai kwamba alikuwa na uchovu tu.

Bwana Odinga alipelekwa hospitalini Jumatatu mchana baada ya kushiriki mkutano wa kisiasa na madaktari wake waliamuru apumzike hospitalini.

Hadi sasa Raila Odinga mwenye umri wa miaka 65 amekuwa ni mtu mkakamavu.

Katika miezi ya hivi karibuni amekuwa akipigia debe katiba mpya inayopendekezwa na hajaripotiwa kuwa na matatizo ya kiafya.

Taarifa ya kupasualiwa kwake imewashangaza wengi.

Hadi sasa , maswali mengi kuhusu afya ya kiongozi nchini Kenya yameelekezwa kwa rais Mwai kibaki.

Baada ya uchaguzi wa mwaka 2003 kulikuwa na tetesi kwamba alipata kiarusi. Hata hivyo maafisa wake walikanusha madai hayo wakisema alikuwa na matatizo madogo tu ya kiafya.

HAPA NA PALE

MWEZI MARCH MWAKA HUU BONGE WA POWERBREAKFAST ALIPODHURU MWANZA KUOMBA SAMAHANI HUKU AKIWAPOZA WANANCHI KWA ZAWADI ZA KALENDA, MOJA KATI YA KERO ALIZO RIPOTI NI SHIMO HILI LILILOKUWEPO KONA YA ASPEN HOTEL KUELEKEA MLANGO MMOJA MWANZA.(tizama picha inayofuata)

BAADA YA ILE STYLE YA KUJAZA KIFUSI CHA UDONGO KUBEZWA KUWA INASHUSHA HADHI YA JIJI NA SI MPANGO ENDELEVU, HATIMAYE BONGE KASIKIKA BWANA, NA SASA SHIMO HALIPO TENA WADAU.

USWAZI NELA (KWA NYUMA HIVI) SIKU HIZI MKEKA SI KITU CHA KUULIZA. NASKIA ETI NI KAMPENI ZA KICHINICHINI ZA WAGOMBEA WA ENEO HUSIKA.

ENEO LA MLANGO MMOJA MABATINI MWANZA AL MAARUFU KWA JINA 'LANGO LANGO' MASHUHURI KWA BIDHAA ZA MITUMBA KUANZIA VIFAA VYA MAJUMBANI HADI MAVAZI. NI KAMA MANZESE VILE AU KARIAKOO.

Monday, June 28, 2010

HAPPY BIRTHDAY TO CEDY AND CATBERT.

MWANANGU MWENYEWE CATHBERT AKIMLISHA BRO WAKE CEDY.

CEDRICK AKIMLISHA KEKI MAMAYAKE MZAZI OLIVER G.SENGO.

KAKA WA PANGANI AKILIONGOZA JAHAZI FRANK, KABAGO, MR. UK NA DJ GEORGE KATIKA MENYUZ!.

YANKIZ AND SISTERZ.

KAMA KAWA ZA USWAZI STORI WAKATI WAKUMANGA, MLO UNASHUKA SWAFIiiii, KULIA KABISA BROTHER GABRIEL LYOTAM WA SAHARA COMMUNICATION, WENGINE MEZANI TEHE TEHE!

SISTERS.

CATHBERT AKIZIMA MSHUMAA KUADHIMISHA MIAKA MIWILI YA KUZALIWA.

FIRST BORN CEDRICK NAYE AKIZIMA MSHUMAA KUADHIMISHA MIAKA MITANO.

FRIENDZ WA FAMILIA WALIOJUMUIKA JANA JUMAPILI.

MASHINDANO YA NGOMA ZA ASILI YA BALIMI KUANZA JULAI 17, 2010

MENEJA WA BIA YA BALIMI FIMBO BUTALLAH AKIZITANGAZA ZAWADI NONO ZA VIKUNDI VITAKAVYO SHINDA.


KAMPUNI YA BIA TANZANIA (TBL) KUPITIA BIA YAKE YA BALIMI EXTRA LAGER LEO IMETANGAZA KWA MARA NYINGINE UDHAMINI WAKE KATIKA MASHINDANO YA NGOMA ASILI KANDA YA ZIWA. MASHINDANO HAYO YANATARAJIWA KUANZA RASMI TRH 17 JULY 2010 KATIKA NGAZI ZA MIKOA AMBAPO MIKOA MITANO ITASHIRIKI, MIKOA HIYO NI MWANZA, SHINYANGA, MARA, KAGERA NA TABORA.
MKURUGENZI WA MASOKO WA TBL DAVID MINJA AMESEMA KUWA BIA YA BALIMI IMEKUWA KIUNGO KIKUBWA KINACHOUNGANISHA TAMADUNI ZA WAKAZI WA KANDA YA ZIWA, HUKU IKITOA FURSA YA PEKEE KWA WAKULIMA KUSHEREHEKEA MAVUNO YAO.

MENEJA WA MAUZO NA USANBAZAJI WA KANDA, KASIRO MSANGI AMEWAOMBA WAKAZI WA MIKOA YOTE KUJITOKEZA KWA WINGI KUPATA BURUDANI NA KUJIKUMBUSHA TAMADUNI ZA MAKABILA YA KANDA YA ZIWA. "BIA YA BALIMI IMEKUWA IKIENDESHA NA KUDHAMINI MICHEZO MINGI KATIKA KANDA YA ZIWA NA TUNAAHIDI KUENDELEZA JUHUDI HIZI" ALISEMA MSANGI.