ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 4, 2010

MASHINDANO YA MITUMBWI YA BALIMI YAFANA.

Fainali za mashindano ya mitumbwi ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra Lager zimefanyika leo katika fukwe za mwaloni jijini Mwanza, washindi kupatikana na kukabidhiwa vitita vya zawadi.

,Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager Fimbo Butallah amesema, Ni zaidi ya miaka mitano sasa, bia ya Balimi imekuwa ikiendesha mashindano haya katika kanda ya Ziwa na mkoani Kigoma, kwa kipindi chote hiki mafanikio yameonekana, licha ya kutoa burudani washiriki wameweza kujipatia kipato cha ziada kupitia zawadi nono zinazotolewa matarajio ya baadaye kuyafanya mashindano yawe sehemu ya utalii.

Mashindano hayo ya kupiga kasia ambayo leo yamefikia tamati, yameshirikisha mikoa ya Kigoma, Mwanza, Mara, Kagera na visiwa vya Ukerewe, huku yakiendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wakazi wa Kanda ya ziwa na wale wa Kigoma kufuatia mashabiki na wapenzi wa mchezo huo kuongezeka mwaka hadi mwaka.

Washindi vinara kwa upande wa wanaume ni kutoka mkoa wa kagera hapa ni pale walipofika ukingoni.

SUGUA KISIGINO!!! Bendi maarufu ya muziki wa Dansi ya African Stars (Twanga Pepeta) wakitoa burudani ya aina yake kwa mashabiki katika fainali za mashindano ya mitumbwi ya Balimi jijini Mwanza.

AAaaah! Balimi inashuka safi ukipiga ndizi na nyama choma.

Mabadiliko ya hali ya hewa yakiambatana na mvua kali katikati ya mashindano hayakubadili chochote ngoma ilisongeshwa, ile hali kwa mashabiki ilikuwa hakuna kutoka mtu.

"Hii mvua ni ya mtu!!" Mr. Msangi akiteta na wadau wenzake wa TBL katikati ni Editha Mushi meneja wa mawasiliano na mahusiano wa kampuni hiyo.

Kikundi cha ngoma asili toka ukerewe nacho kilialikwa kutia nakshi mashindano, Wanakatika haoOOO!!

Palikuwa hapatoshi kwani watu walimiminika haswaa.

Kapteni wa Washindi wa kwanza wanaume Thobias Kaichum Toka bukoba akichukua zawadi sh milioni mbili na nusu.

Kapteni wa Washindi wa kwanza wanawake Salome Ernest toka bukoba akichukua zawadi sh milioni mbili, nafasi ya pili Mwanza ikachukuwa milioni mbili, nafasi ya tatu ikaenda Ukerewe nao wakakamata kitita cha milioni moja na nusu.

Kapteni wa Washindi wa pili wanawake Yunus Lewis toka Ukerewe akikabidhiwa kitita cha sh milioni moja na nusu, nafasi ya 3 ilichukuliwa na washiriki toka Mwanza laki saba na nusu, nafasi ya 4 ilikwenda Ukerewe laki tano,huku nafasi ya 5 ikienda tena Bukoba laki mbili.

Dj Ommy jr akinogesha Shughuli ndani ya Mashindano hayo yaliyoanza saa 3 asubuhi na kumalizika majira ya jioni, yalishirikisha timu tano toka kila kituo kilichoshiriki ngazi ya awali toka mikoa ya yote mitano ya kanda ya ziwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.