ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 16, 2010

MCHUJO WA GIRAFFE UNIQUE MODEL 2010 NI JUMAMOSI HII SAA SITA MCHANA

Mchujo wa kuwatafuta wanamitindo wenye sifa za kitofauti yaan i" Giaffe unique model " utafanyika jumamosi hii ya tarehe 20 mwezi wa kumi na moja katika hoteli yenye hadhi ya nyota nne Giraffe ocean view hotel katika ukumbi wa jet 1.

Akiongea na blog zote maarufu nchini Tanzania mratibu wa shindano hilo bwana Magese Methuselah Magese amesema kuwa shindano hilo ni la kizalendo lenye nia mahususi ya kukuza tasnia ya mitindo na wanamitindo wachanga nchini Tanzania kwa kuleta umoja,mafanikio na kuhimiza mapinduzi ili tasnia hii iwe ajira kamili kwa wanamitindo wa hapa nchini kinyume na ilivyo sasa.

Ameongeza kuwa ikiwa vyombo vya habari vitaunga mkono mapinduzi haya kwa kutangaza kwa wingi habari za mitindo, wamamitindo na wabunifu wa ndani, itageuza mtazamo wa watanzania wengi kuondokana na utamaduni wa kuvaa nguo kutoka nje ya nchi pekee badala yake wapende kuvaa nguo zilizobuniwa na wabunifu wa Tanzania.

" Hii itachangia wabunifu kuwa na kipato kikubwa na maonyesho ya mavazi yatakuwa mengi ambapo wanamitindo watafaidika kwa kulipwa kwa kiwango chajuu, aidha vyombo vya habari vikitangaza sana tasnia hii jamii itapenda zaidi hata makampuni mengi yatajitokeza kuwekeza na kujitangaza kwa kudhamini shughuli za mitindo nchini Tanzania kitu ambacho kitaongeza pato la taifa na kpato cha mtu mmojammoja.

Wito umetolewa kwa wasichana wote wenye sifa na vigezo vya kushiriki shindano hilo lenye hadhi ya kitaifa kujitokeza kwaajili ya mchujo tarehe 20 novemba saa sita mchana katika hoteli hiyo iliyopo maeneo ya africana mbezi beach ambapo majaji watakuwa Steven Kanumba, Miriam Gerald, Ali Remtulah, Vitoria Martin na Asia Idarous, watakao shiriki kuchagua wasichana kumi bora wataoingia moja kwa moja katika shindano hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.