ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 8, 2010

CHEREKO-CHEREKO SAFARI HII NI JORAM & GRACE

SI WAWILI TENA BALI NI MWILI MMOJA, HILO ANDIKO LIMEJIDHIHIRISHA TENA NA SAFARI HII NI KWA VIJANA WAWILI JORAM NGAIZA NA GRACE MTONGOLE AMBAO WAMEFUNGA PINGU ZA MAISHA MWISHONI MWA WIKI KATIKA KANISA LA KIKATOLIKI NYAKAHOJA MJINI MWANZA.

BWANA HARUSI AKIMLISHA KEKI BI HARUSI NDANI YA SHEREHE SAFI YA KUWAPONGEZA ILIYOFANYIKA JIONI YA SIKU HIYO HIYO YA NDOA PALE YATCH CLUB.

NI MGENI GANI WA KWANZA UNGEPENDA AWE MGENI WA KWANZA KUTEMBELEA NYUMBA YENU? JORAM AKAMCHAGUA BINTI HUYU MDOGO. WATU WAKAGONGANISHA VIGANJA PWAAH! PWAAH! PWAAaa!

HATUA ZA MINATO KUELEKEA KWENYE MENUz. PLIZ UTANISAMEHE MISOSI SINTOKUONYESHA USIJE JILAUMU KWANINI HUKUPATA MWALIKO.

SI MCHEZOo!

HAPA JEH!

BURUDANI PALE KATI WOW! THE WACO J. FROM UGANDA.

MARA ZOTE KATIKA FAMILIA FURAHA YA KILA MMOJA HUPIMWA KWA MIZANI YAKE, LAKINI USHAPIMA KIWANGO CHA FURAHA ANAYOKUWA NAYO DADA PINDI KAKA ANAPOPATA JIKO? MBALI NA KUJITAHIDI KILA KITU KIENDE SAWA, FURAHA YA DADA HAITOFAUTIANI NA YA MAMA. PICHANI MWENYE GAUNI SAFI NA POCHI AINA YA KIPIMA JOTO NI DADA WA BWANA HARUSI ANAITWA....(msaada jamani)

KILA LA KHERI KWA MR&MRS JORAM NGAIZA. NA BURUDANI IENDELEE!!!!

Tupe maoni yako

4 comments:

  1. Harusi ilifana bi harusi 'grace' ulipendeza sana naona unachekelea sana mpk keki inataka kudondoka basi na iwe ivyo ndani ya nyumba yenu vicheko viendelee mpk mwisho wa maisha yenu.....nawatakia kila la kheri ktk ndoa yenu May lord give u love,happiness and live a healthier life ever....alice harare mapuli...from dar

    ReplyDelete
  2. Mmependeza sana jamani nawatakia maisha yenye furaha milele yote.

    ReplyDelete
  3. Kila la Kheri kati maisha yenu mapya wapedwa mungu awatangulie katika kila jambo.G sengo bigup kwa kutuletea matukio motomoto

    ReplyDelete
  4. Mmeendana sana jamani,Mwenyezi Mungu awabariki na ninyi kuzidi kukumbuka ahadi mlizowekeana mbele la hekalu la Mungu Baba,Mwana na Roho Mtakatifu.
    Amen.Bwana awe nanyi wapendo.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.