ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 7, 2010

SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 30 YA TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU KITUO CHA MWANZA.


MH. MKUU WA MKOA WA MWANZA ABBAS KANDORO AKITOA HOTUBA YA UFUNGUZI WA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAK 30 YA TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU KITUO CHA MWANZA TRH 7 OCT 2010.
MH ALIONA MENGI YENYE KUSTAHILI SIFA NA AKASEMA NI JAMBO LA KUJIVUNIA KUONA KUWA TANGU KUANZISHWA KWA KITUO HIKI KIMEWEZA KUFANYA TAFITI MBALIMBALI ZINAZOJULIKANA KIMATAIFA AMBAZO PIA ZIMETOA MCHANGO MKUBWA KTK KUIMARISHA SERA.


MOJA WAPO YA UTAFITI WA KIMATAIFA NA KUWEZESHA MATOKEO YAKE KUTUMIKA KUTENGENEZA SERA NI ULE ULIOBAINI KUWA UKIDHIBITI MAGONJWA YA KUJAMIIANA UNAPUNGUZA KASI YA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KWA 40%. UTAFITI ULIOFANYIKA MWANZA .KUANZIA 1991 HADI 1994 NA KUHUSISHA WASHIRIKI WAPATAO 12,000.

KAIMU MKURUGENZI NIMR MWELE MALECELA AKIZUNGUMZA NA VYOMBO VYA HABARI NA ALIYEKETI PAMBENI YAKE NI MKUU WA KITUO CHA UTAFITI MWANZA.

MEZA KUU.
KITENGO HIKI CHA UTAFITI KIMEAHIDI KUTOA MATOKEO KWA LUGHA YA KUELEWEKA ILI WANANCHI WOTE WAJUE KILICHOFANYIKA KWA KIPINDI CHOTE CHA UTAFITI CHA MIAKA 30 NA YALE YATAKAYO JIRI KTK TAFITI ZINAZOKUJA.

JENGO LA NIMR MWANZA.
MOJA KATI YA TAFITI TATU AMBAZO ZIMEWEZA KUORESHA SERA NA HUDUMA NI ILE YA TIBA NA DALILI KWA AJILI YA MAGONJWA YA ZINAA AMBAPO UTAFITI UMEONYESHA KUWA TOHARA KWA WANAUME INAVYOWEZA KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI NA HATIMAYE KITENGO KUSABISHA UANZISHWAJI WA SERA MPANGO WA KUFANYA TOHARA NCHI NZIMA.

KITUO CHA NIMR MWANZA KUPITIA UTAFITI WAKE KIMEWEZESHA MATIBABU YA UGONJWA WA KASWENDE KWA AKINA MAMA WAJAWAZITO, UGONJWA ULIOKUWA UKIWALETEA MATATIZO KWA AFYA YA MAMA NA MTOTO, UTAFITI HUO TAYARI UMEONYESHA KWAMBA VIPIMO VYA PAPO HAPO VILIVYOTENGENEZWA MIAKA YA HIVI KARIBUNI VINAFAA NA MGONJWA ANAWEZA KUPATA MAJIBU SIKU HIYO NA KUANZA MATIBABU TOFATI NA SIKU ZA NYUMA AMBAPO MGONJWA ALILAZIMIKA KUSUBIRI KWA SIKU ZAIDI YA MBILI KABLA YA KUPATIWA MAJIBU.

AMEWASIHI WATAFITI HAO WA NIMR KITUO CHA MWANZA KUTOBWETEKA NA MAFANIKIO WALIYOYAPATA BALI KUENDELEA KUCHAPA KAZI KWA BIDII ILI KULILETEA HESHIMA TAIFA HILI.

MKUU WA MKOA WA MWANZA KATIKA STORI ZAKE ALIZUNGUMZIA ILE TABIA YA KUPENDA CHIPS MAYAI KWA SANA AU PILAU UNAKAMUA MAFUTA YANACHURUZIKA MKONONI HADI KWAPANI TUNAFURAHIA AKASIHI TUACHANE NAYO. TULE CHAKULA BORA, TUZINGATIE KANUNI ZA AFYA TUFANYE MAZOEZI NA KUHAKIKISHA KUWA TUNAISHI KTK MAZINGIRA MASAFI.

WASHIRIKI WA UFUNGUZI WA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 30 YA TAASISI YA TAIFA YA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU KITUO CHA MWANZA.

KATIKA MAADHIMISHO HAYO VYETI VYA KUTAMBUA HUDUMA WALIYOIFANYA KUTUMIKIA TAASISI YA UGONJWA WA MATENDE VILITOLEWA. PICHANI NI ELIZABETH BUGUMBA AKIPOKEA CHETI CHAKE TOKA KWA MGENI RASMI.

JAMAA MASHUHURI SANA WILAYA YA UKEREWE DR. MASHAURI.

ANTHONY SITENGA WA KITENGO CHA KARAKANA AKIPOKEA CHETI CHAKE.

KAIMU MKURUGENZI NIMR MWELE MALACELA AMESEMA KUWA OPEN DAY ZITAFANYIKA KATIKA MAENEO YA VIWANJA VYA NIMR NA HIVYO ANAWAKARIBISHA WANANCHI WOTE WALIO JIJINI MWANZA KUFIKA NA KUONA KAZI ZA TAFITI ZIFANYWAZO.

KILELE CHA MAADHIMISHO HAYO KITAKUWA TRH 20 0CT 2010 AMBAPO MAONESHO NA HAFLA VITAFANYIKA MAKAO MAKUU DAR ES SALAAM.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.