ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 14, 2010

MIUJIZA YATENDEKA CHILE, HATIMAYE WACHIMBAJI WOTE 33 WALIONASA WAOKOKA.

ILE NDOTO YA KUTISHA ILIYOCHUKUWA SIKU SABINI KUMALIZIKA HATIMAYE IMEFIKIA TAMATI KWA HARAKA TOFAUTI NA WENGI TULIVYODHANI HUKU IKISALIMISHA ROHO ZA WATU WOTE 33 WALIFUKIWA NA KIFUSI HUKO KATIKA MIGODI YA SAN JOSE NCHINI CHILELUIS URZUA MCHIMBAJI WA MWISHO KUOKOLEWA AKISHEREHEKEA MBELE YA RAIS WA CHILE SEBASTIAN PINERA MARA TU BAADA YA KUOPOLEWA TOKA KIFUSINI.

Rais wa Chile amesema kamwe nchi yake haitarejea hali iliyokuwa nayo awali baada ya kukamilika kwa shughuli ya uokoaji wa wachimba migodi 33 waliokuwa wamenaswa chini ya ardhi kwa siku 69. Sebastian Pinera amesema anahisi wananchi wa Chile sasa "wana umoja zaidi na imara kuliko wakati mwingine wowote" na wanaothaminika kote duniani.

MCHIMBAJI WA 21 KUOKOLEWA YONNI BARIRIOS AKIPOKEA BUSU MOTO MOTO MARA TU ALIPOIKANYAGA ARDHI.

Kulikuwa na kila hali ya ushangiliaji wakati Luis Urzua, mwenye umri wa miaka 54, mchimbaji wa mwisho alipotolewa nje ya mgodi huo.

WANANCHI WA CHILE WAKISHEREHEKEA WAKATI MTU WA MWISHO ALIYE NASA AKITOLEWA.

Baadhi yao wamebainika kuwa na matatizo ya meno, na wengine wanasumbuliwa na macho kutokana na kuishi katika vumbi na giza mgodini humo. Mmoja wao amegundulika kuwa na kichomi, ingawa hali yake inaelezewa kuwa si mbaya sana.
Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Jaime Manalich, alisisitiza kuwa wachimbaji wote wanaonekana kuwa katika afya njema kuliko ilivyokuwa ikitarajiwa. Haijawahi kutokea binadamu aliyenaswa chini ya ardhi kwa muda mrefu kiasi hicho kusalimika.
Wachimbaji hao walikuwa wamesalia na chakula cha kutosheleza kwa saa 48 wakati sehemu ya mgodi wa shaba na dhahabu wa San Jose nchini Chile katika jangwa la Atacama ulipoanguka tarehe 5 Agosti. Baada ya siku 17 za kuchimba kuwatafuta, hatimaye waokoaji walifanikiwa kuwasiliana nao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.