ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 18, 2010

TUKIO HILI LIMETOKEA HUKO MKOANI SINGIDA.

KIBAKA mmoja ambaye hajafahamika jna lake wala makazi ameuawa kikatili na wananchi wenye hasira kali na kisha kuchomwa moto baada ya kufanya jaribio la kuvunja duka na kuiba bidhaa mbalimbali. Tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia juzi majira ya saa 10 alfajiri katika eneo la Mwenge Manispaa ya singida ambapo kibaka huyo alikuwa na wenzake watano.

Hata hivyo wananchi wa maeneo ya jirani wamesema kuwa hiyo ni mara ya tatu kwa duka hilo kuvamiwa na vibaka na kisha mali kuchuliwa ambapo mwenye duka hiloa akiamka asubuhi anakuta duka jeupe na hivyo kumpunguzia nguvu kazi ya kujiletea maendeleo yake pamoja na familia yake. "Jamani sisi tumechoshwa na hawa wezi kila mara wanamwibia huyo kijana wa hili duka hebu angalieni mali yote imetolewa nje na kama sio kushiuka si angekuta hana kitu, tunasema tukikamata kibaka safai hii aaangalie mfano wa huyu mwenzao hatuna msaliamtume, polisi watakuja kuchukua majivu tu."Alissisistiza mama mmoja jirani na eneo hilo la tukio.


PICHA NA HABARI KWA HISANI YA BLOG YA FULL SHANGWE.

Blog hii inaungana na wadau wote wa habari kulaani matukio kama haya ya sehemu ya kundi la watu kujichukulia sheria mkononi na kusabisha madhara kwa wengine ikiwemo na kupoteza uhai wa muhisika, hali hii inapaswa kupigwa vita kwa nguvu zote.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. Inasikitisha lkn wakati mwingine ni sawa tu make hawa huwa balaaa wakikuwahi. Mfn ni dj kid walivyomtenda.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.