ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, September 9, 2010

MRADI WA CHAMPION WATETA NA WADAU JIJINI MWANZA MENGI YAIBULIWA, WADAU WAJIFUNZA.

ULE MRADI UNAUNAOLENGA KUHAMASISHA MJADALA WA KITAIFA KUHUSU MAJUKUMU YA WANAUME NA KUONGEZA USAWA WA KIJINSIA HIVYO KUPUNGUZA HATARI YA WANAUME, WANAWAKE NA WATOTO KUPATA VVU\ UKIMWI NA KUPUNGUZA MATOKEO YA ATHARI ZINGINE MBAYA ZA AFYA YA UZAZI, MRADI HUO LEO UMETINGA JIJINI MWANZA KUZUNGUMZA ANA KWA ANA NA WADAU WA HABARI.

KAMPENI YA MAWASILIANO BAINA YA WAPENZI IMEANZISHWA BAADA YA TAFITI KUFANYWA NA KUONYESHA KUWA KUNA TATIZO LA MAWASILIANO BAINA YA WATU WALIOPO KWENYE MAHUSIANO YA KIMAPENZI KAMA NDOA TATIZO LINALOPELEKEA KUTORIDHIKA HIVYO KUWA NA MAHUSIANO NA WAPENZI WENGI CHANZO CHA MAAMBUKIZI YA VVU.

KWA NINI INAFIKIA WAKATI UNAJUTA KUZALIWA MWANAMKE?
MAJIBU YA WENGI:
-pingamizi ya haki hata kama ni juu ya suala dogo lenye maamuzi juu ya mwili wako.
-kutokuwa na maamuzi katika familia pindi nitakapoolewa.
-nabeba mimba nailea, mtoto anazaliwa, nasimamia malezi mpaka anakuwa mwisho wa siku nikiachana na mwanaume 'mtoto mali ya mwanaume'


MSANII WA MUZIKI WA KIZAZI KIPYA BEATRICE NAYE ALIREJEA NYUMBANI MWANZA KUUNGANA KUHAMASISHA JUU YA MPANGO MZIMA WA KUVUNJA UKIMYA.

MAMBO MENGI YALIIBULIWA KATIKA MDAHALO HUO, HITIMISHO LIKAWA:
-mawasiliano ni muhimu katika kudumisha upendo na furaha ktk mahusiano.
-mawasiliano mazuri hujenga ushirikiano ktk familia.
-mawasiliano mazuri ni yale yenye uwazi kuthaminiana na kusikilizana.


UNGEJIBUJE KWA SWALI HILI: JE UNAJUTA KUZALIWA MWANAUME?

MR MATAGIRI TOKA MPANGO WA KULINDA ZIWA VICTORIA AMECHANGIA KUWA MILA NA DESTURI NA KUOGOPA KUONEKANA KAMA SIYO MWANAUME NI MOJA YA VIKWAZO KATIKA MAWASILIANO.

PICHA YA PAMOJA WADAU WA CHAMPION MWANZA WALIO FANIKISHA ZIARA HIYO.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.