ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 20, 2010

AFYA YA KID BWAY YAENDELEA KUIMARIKA.

Afya ya mtangazaji wa radio FREE AFRIKA KID BWAY inaendelea kuimarika kadri anavyoendelea kupata matibabu katika hospitali ya Bugando jijini Mwanza.

Maendeleo ni ya kuridhisha yanayotia matumaini makubwa sana tofauti na awali. Kwa hivi sasa mshkaji anaweza kula mwenyewe ingawa chakula anachotumia ni kile rojorojo kama uji, supu na vyakula vilivyopondwapondwa kwani nguvu ya taya kutafuna inampa maumivu.

Kutokana na maumivu ya kichwa anapatiwa dawa maalum na amepewa ushauri kuwa asifanye maongezi zaidi ya kujuliwa hali na kusikilizwa juu ya huduma anayohitaji, pia anapaswa kupumzika muda mwingi, hivyo amekuwa akishinda kitandani akiwa amelala.

Nimepata fursa ya kuzungumza na mmoja wa madaktari wa hapa ameniarifu kuwa bahati iliyoje kuna madaktari wataalamu wa upasuaji kutoka nchi za mbali ambao wamekuja kitambo sasa kwa ajili ya kutoa huduma za upasuaji bure nao wamemtembelea na kumfanyia uchunguzi na wamemweka katika ratiba na sasa wako katika mikakati ya kumpa huduma, ingawa daktari hajanitamkia wazi kwamba wameona nini na watakwenda kufanya nini. Lakini kwa ufupi hali inaridhisha.

Tupe maoni yako

2 comments:

  1. Uncle mpe pole sana mshikaji, natumaini mungu atamsaidia apate nafuu mapema.

    Uncleeeeeeeeeeeeeeeeeh!

    ReplyDelete
  2. Tumuombe sana mshkaji aweze kupona that's all about

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.