ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, August 20, 2010

MWANANCHI WILAYANI TARIME AUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA ASKARI POLISI .

Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya ASP Costatine Massawe amesema kuwa tume imeundwa kwa ajili ya kufanya uchunguzi ambapo amekiri kuwa marehemu James ameuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi huko Kinesi wilayani Rorya mkoani Mara.




JAMES JOSEPH ALIYEUAWA NA ASKARI.

ASP Massawe amesema kuwa ,James aliuawa kwa kupigwa risasi na askari kwa madai ya kuthubutu kumnyan’ganya silaha ya Bunduki moja kati ya polisi waliomweka chini ya ulinzi wilayani Rorya Mkoa wa Mara tukio lililotokea marehemu akiwa katika nyumba ya wageni iitwayo Silent Inn Bar and Guest house mnamo agosti 12 saa 11 jioni ambapo siku iliyofuata ya agosti 13 alifikishwa katika hosptali ya Wilaya na kufanyiwa uchunguzi ili apate kuzikwa ambapo hakuzikwa hadi leo hii.

“Nimepokea simu nyingi toka kwa watu mbali mbali wakiuliza ni risasi ngapi zilizoua lakini mimi kwa sasa siwezi kuzungumzia swala hilo kwani tayari tume nimeisha anza uchunguzi tangu jana na tayari baba wa marehemu ameshatoa maelezo mimi nasuburi tume ikamilishe uchunguzi wake. Tume hiyo inahusisha wanasheria pamoja ofisi ya polisi makao makuu na ikikamilika mwanasheria wa Serikali atatoa taarifa na taratibu nyingine zitafanyika” alisema.

Hatua zote hizi zinzfanyika IKIWA leo ni siku ya 8 mwili wa marehemu James Joseph Mag’ancha (25) bado ukiaendela kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hosptali ya wilaya mjini Tarime kufutia familia ya marehemu kutoridhika na uchungunzi uliofanywa awali.

Hata hivyo uchunguzi mwingine ulifanyika upya agosti 17 katika chumba cha kuhifadhia maiti mbele ya baba mzazi wa marehemu, mama mdogo, daktari pamoja na ASP Massawe ambapo bado wazazi hawakuridhika kufatia mabishano juu ya matundu ya risasi ambapo kamanda alidai ni matundu mawili, lakini baba mzazi alisema ni zaidi ya mawili hivyo hali hiyo ikapelekea kuundwa upya kwa tume huru ya kipolisi iliyoanza rasmi uchunguzi juzi agosti 18.

Baba mzazi wa Marehemu, mzee Joseph Mag’ancha aliwambia waandishi wa habari juzi kuwa hatamzika marehemu mpaka atakopofika kijana wake mkubwa ambaye ni mwanajeshi aishie Dar es salaam ili kusaidiana nae kuhakikisha kuwa uchunguzi unafanyika kwa haki.

Maga’ncha amesema kuwa mwanae hakuwahi kuingia katika jeshi lolote kama inavyodaiwa kuwa aliwahi kuingia JKT, vile vile alikanusha mwanae huyo kuwa na upungufu wa akili kama ilivyodaiwa ambapo amesema kuwa mwanae alikuwa na akili timamu na siku zote alikuwa akifanya biashara ndogondogo (machinga) na kipindi chote alikuwa akiishi Jijini Dar es salaam.

Mauti hayo yamemkuta kijana James kipindi ambapo baba mzazi alimwita toka jijini Dar es salaam kuja kujenga kaburi la mama yake mzazi pamoja na bibi yake mzaa mama yake, ambapo siku ya kutiko tayari alikuwa amekwisha nunua matofari ,mchanga pamoja na simenti na kuongeza kuwa marehemu ameacha mke na watoto wawili.

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. jeshi letu kaka linakera sana
    mungu amlaze mahala pema peponi.AMEN.

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.