ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 14, 2010

SIKU YA WACHANGIA DAMU DUNIANI KITAIFA MWANZA YAFANA.

WORLD BLOOD DONORS DAY.
WAKAZI WA JIJI LA MWANZA LEO WAMEKUTANA KATIKA VIWANJA VYA GHAND HALL KUADHIMISHA SIKU HII PAMOJA NA KUSHIRIKI ZOEZI LA UTOAJI DAMU SALAMA. PICHANI MC WA MAADHIMISHO HAYO YALIYOFANYIKA KITAIFA MWANZA AFISA UHUSIANO WA JIJI BW JOSEPH MLINZI AKIHUSIKA NA RATIBA.

VIONGOZI WA SIASA, KAMATI YA MAANDALIZI, VIONGOZI WA DINI NA WAGENI WAALIKWA MEZA KUU.

KAULI MBIU YA MAADHIMISHO YA MWAKA HUU NI "WACHANGIAJI DAMU VIJANA, DAMU MPYA KWA DUNIA YA LEO" NAO VIJANA WALIWAKILISHA KISAWA SAWA.

BURUDANI NAYO ILIKUWA NA SEHEMU YAKE.

MSTARI KUELEKEA KATIKA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU. TAKWIMU ZINAONESHA KUMEKUWEPO NA ONGEZEKO LA UKUSANYAJI WA DAMU MWAKA HADI MWAKA HALI INAYOPELEKEA UHAKIKA WA KUWAPO KWA DAMU YA KUTOSHA MAHOSPITALINI.

KABLA YA MWANANCHI KUCHANGIA DAMU, SAMPLE YA DAMU HUCHUKULIWA NA KUPIMWA NDIPO MAAMUZI YA KUTOA AU KUTOTOA HUFANYIKA.

WAWEZA KUWA NA DAMU SAFI LAKINI AFYA IKAWA NA UTATA, HIVYO LAZIMA TUPIME PRESHA NA MENGINE...

NCHINI PETU VIFO VINGI HUTOKEA KUTOKANA NA UKOSEFU WA DAMU, MOJA YA MAKUNDI YANAYOATHIRIKA ZAIDI NI AKINA MAMA WAJAWAZITO WAKATI WA MIMBA NA KUJIFUNGUA. KWA ZOEZI KAMA HILI VIFO VINAWEZA KUZUILIKA.

ASKARI WA JESHI LA WANANCHI TANZANIA (JWTZ) NAO WALIJITOKEZA. WAKATI NIKICHUKUWA PICHA NIKAULIZA SWALI KIMTINDO:-
"AKITOKEA MKUU HAPA YALE MAMBO YETU YA SALUTI INAKUWAJE?"
"HA-HA-HA-HAAAA!!!!" (WAKAANGUA KICHEKO)


BAADHI YA VIJANA WENYE SIFA ZA KUCHANGIA DAMU WALIO HUDHURIA ZOEZI HILO WAKIPONGEZANA KWA STORI HUKU WAKILAMBA CLUCOSE.

PAMOJA INAWEZEKANA CHANGIA DAMU MARA KWA MARA, OKOA MAISHA.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.