ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, January 4, 2010

MV. BUTIAMA HATARINI ZIWA VICTORIA.

PICHANI WAANDISHI WA HABARI WA VYOMBO MBALIMBALI WAKISAKA NEWS BILA MAFANIKIO KATIKA OFISI ZA MAOFISA WA KAMPUNI YA MARINE SERVICE MWANZA WANAOMILIKI MELI HIYO.
MELI YA MV.BUTIAMA IMEKWAMA LEO ZIWANI VICTORIA MARA BAADA YA KUPIGWA NA DHORUBA KALI NA KUZIMIKA INJINI.TUKIO HILI LIMETOKEA KARIBU NA KISIWA CHA MAKOBE MWENDO WA SAA TANO NA DAKIKA 18 ASUBUHI IKIWA NI SAA MOJA MARA BAADA YA KUANZA SAFARI KUTOKA WILAYA YA UKEREWE KUELEKEA JIJINI MWANZA. MELI HIYO IKIWA INASUKUMWA NA UPEPO HUKU IKIKABIRIANA NA MAWIMBI MAZITO YA MAJI IMEKOKOTWA HADI ENEO LA KARIBU NA MWAMBAO WA IGOMBE. MARA BAADA YA HALI HIYO KUTOKEA HUKU MVUA KUBWA IKINYESHA NA UPEPO MKALI UKIVUMA ZIWANI HUMO ABIRIA WALICHANGANYIKIWA WASIFAHAMU KINACHOFUATA KWANI ILICHUKUA MASAA MATATU TANGU TUKIO HILO KUTOKEA NA KUSIWE NA MSAADA WOWOTE WALA JITIHADA ZOZOTE TOKA KWA VYOMBO HUSIKA (INASIKITISHA). SABABU ZA MISUKOSUKO HIYO ZINATAJWA KUWA NI MELI HIYO KUBEBA ABIRIA NA MIZIGO ZAIDI YA UWEZO WAKE, KIASI CHA ABIRIA WENGI KUSIMAMA. JANA MELI HIYO ILISHINDWA KUFANYA SAFARI ZAKE KUTOKANA NA KUWA NA HITILAFU HALI NA HAIJAFAHAMIKA KAMA KWELI MELI HIYO MARA BAADA YA MATENGENEZO KAMA ILIKAGULIWA NA WADAU WA CHOMBO CHA KUDHIBITI USALAMA WA VYOMBO VYA USAFIRI MAJINI NA NCHI KAVU (SUMATRA). KIASI CHA SAA NANE NA DAKIKA 30 MELI YA CLARIAS NA BOTI ZA JESHI LA POLISI MAJINI TAYARI ZIMEFIKA ENEO LA TUKIO KUFANYA UOKOAJI. Tukio hili na lile la MV.Bukoba karibu kuwa dugu moja. HATARI LAKINI SALAMA

Tupe maoni yako

1 comments:

  1. Njia ngumu zaidi ya kujifunza ni ile tujifunzayo kutokana na makosa. Sasa ukiona kuwa hata kwa makosa hayohayo wapo wasiotaka ama kuweza kujifunza, unajiuliza kama akili zetu zina akili ama la!!!
    Ni Mwanza hiyohiyo iliyoshuhudia Mv Bukoba na wanajua chanzo. Ni Mwanza hiyohiyo inayoshindwa kukarabati Mv Butiama na kuwaweka wasafiri kwenye hatari kama ya Mv Nukoba. Na sio Butiama tu, nakumbuka mwaka 2000 Mv Victoria ilituzimikia kwa takribani saa nzima dk chache baada ya kutoka Mwanza. Hiyo ilikuwa siku kadhaa kabla ya Xmas na kwa hakika tuliogopa saana. Najaribu kupiga picha hawa waliozimikiwa kwa dhoruba na walikuwa WAMERUNDIKWA.
    Sipati picha
    Asante kwa kutuunganisha na Kanda ya Ziwa
    Blessings

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.