ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 5, 2009

MSIBA WA MWENYEKITI CLOUDS RATIBA YA FIESTA YABADILIKA


Tamasha la Fiesta One Love 2009 lililotarajiwa kufanyika jumamosi hii,Novemba 7 katika uwanja wa posta,kijitonyama jijini Dar,limeaihirishwa na kusogezwa mbele.

Akitoa maelezo hayo mratibu mkuu wa tamasha hilo Bw.Ruge Mutahaba amesema kuwa tamasha hilo limeaihirishwa hadi Novemba 21 na mabadiliko hayo yanatokana na wahusika wakuu wakiwemo wafanyakazi wa Clouds Media Group/Prime Time Promotions (ambao kwa kiasi kikubwa ndiyo waandaji wa tamasha hilo) kuondokewa Mwenyekiti wao Mzee Alex Mkama Kusaga aliyefariki nchini Afrika ya Kusini alikokwenda kupata matibabu.

Mutahaba amesema ratiba ya wasanii wambao walipaswa kushiriki kwenye tamasha hilo la Kitaifa iko pale pale wala haijabadilika,na kwamba msanii ambaye alitajwa angewatumbuiza wakazi wa Dar kutoka chini Marekani kwenye tamasha hilo,Buster Rhymes na wenzake naye ratiba yake iko pale pale,kwamba atakamua vilivyo siku hiyo.

Aidha kwa taarifa za msiba wa Mzee K. inaelezwa kuwa mwili wake utawasili leo saa 1 na kupelekwa hospitali ya Lugalo. ibada ya mazishi itafanyika siku ya jumamosi trh 7/nov saa 5:30 hadi saa 7:30 katika kanisa la azania front na baadaye mazishi ktk makaburi ya kinondoni Dar es salaam msiba upo nyumbani kwake karibu na Girrafe Hotel,kuhusu ratiba zaidi tutaendelea kufahamisha.