ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, June 12, 2009

CHRISTINA SHUSHO NA UJUMBE UNAOJENGA


KUNA MWIMBAJI MKONGWE KTK MUZIKI WA INJILI ALIYEPATA KUTAMBA MIAKA YA 90 HAPA NCHINI TANZANIA NA AFRIKA MASHARIKI KWA UJUMLA AITWAYE MUNIS, YEYE NDANI YA MOJA YA NYIMBO ZAKE ALISEMA "ULIMI KIUNGO KIDOGO MATATIZO YAKE NI MAKUBWA" NAMI NAONGEZA "KAULI NI SILAHA KALI KULIKO BOMU" KWANI INAWEZA KUSAMBARATISHA NAKUTEKETEZA UWEPO WA KILICHOKUWA HAI.
+ IKITUMIWA VIZURI -INAONDOA CHUKI NA KUWEKA UPENDO NA ANANI.
+ LAKINI KINYUME CHAKE - HUBOMOA
"KUNA WATU WAMEKATA TAMAA YA MAISHA KWA SABABU TU WALIAMBIWA hawawezi, PIA KUNA WALIOTIWA MOYO KIPINDI WAKIJIKONGOJA LEO HII WAPO matawi ya juu".
+ EWE RAFIKI NAKUPA ZAWADI KAUSIKILIZE WIMBO "UNIKUMBUKE" WA MWIMBAJI WA MUZIKI WA INJILI CHRISTINA SHUSHO KISHA NAMBIE........

Thursday, June 11, 2009

WALIOWAHI KUWA WAKUU WA MKOA WA MWANZA TANGU UHURU

1. RICHARD SAMURA MABURA (1961-1963)
2. JOHN SAMUEL MALECELA (1963-1965)
3. JOSEPH KIZURIRA NYERERE (1965-1967)
4. JOSEPH NAMATA (1967-1969)
5. OMAR MUHAJI (1970-1972)
6. LAWI NANGWANDA SIJAONA (1972-1975)
7. PETER ABDALLAH KISUMO (1975-1977)
8. BRIGEDIA MUHIDIA KIMARIO (1977-1979)
9. ABDULNURU SULEIMAN (1979-1981)
10.DANIEL MADAHA MACHEMBA (1981-1987)
11.TIMOTHY SHINDIKA (1987-1992)
12.PHILIP JAPHET MANGULA (1992-1993)
13.ERNEST KISUMO NYANDA (1993-1994)
14.DK.FERDINAND SHIJA (1994-1995)
15.MEJA JENERALI JAMES LUHONGA (1996-1999)
16.STEPHEN JOSHUA MASHISHANGA (1999-2003)
17.DANIEL OLE NJOLAY (2003-2006)
18.DK.JAMES ALEX MSEKELA (2006-2009)
19.ABBAS KANDORO(2009- )

DECI NYINGINE YAPIGWA STOP

SERIKALI WILAYANI BUNDA MKOANI MARA IMEAGIZA KAMPUNI MOJA INAYODAI KUSAIDIA WANANCHI MISAADA MBALIMBALI BAADA YA KUCHANGIA FEDHA ZAO, IKIWEMO KUSOMESHA WATOTO HADI ELIMU YA JUU NA KUWAJENGEA NYUMBA NA SHULE WANACHAMA WAKE, KUACHA MARA MOJA SHUGHULI ZAKE MPAKA HAPO ITAKAPOKUWA IMEJIRIDHISHA KAMA SIYO YA KITAPELI.
+ AGLZO HILO LIMETOLEWA JUZI NA KATIBU TAWALA (DAS) WA WILAYA YA BUNDA, DEO MANGAZENI WAKATI AKIZUNGUMZA NA WAWAKILISHI WA ASASI NA MASHIRIKA YASIYOKUWA YA KISERIKALI MJINI BUNDA.
+ KAMPUNI ILIYOPIGWA STOP NA SERIKALI INAJULIKANA KWA JINA LA PEOPLES UNITY FOR DEVELOPMENT IN AFRICA (PUFDIA) INAYOFADHILIWA NA MTANDAO WA KIKRISTO DUNIANI CHINI YA BW. TURKO SIMON WA MAREKANI.
+ KAMPUNI HIYO INAYODAIWA KUSAIDIA WANANCHI KWA MASHARTI NAFUU ILI WAONDOKANE NA UMASKINI KWA KUCHANGIA KIASI KIDOGO CHA FEDHA TAYARI ILIKUWA IMEPATA OFISI NA KUANZA KUTOA MATANGAZO KWA NJIA YA KIPAZA SAUTI NA VIPEPERUSHI.
+MOJA KATI YA VIPENGELE VILIVYOMO KWENYE VIPEPERUSHI HIVYO VINASEMA := ILI MWANANCHI AJENGEWE NYUMBA ANATAKIWA KUTOA KUPANDA KIASI CHA SH 470,000 TU.
++ KAA CHINI TAFAKARI++

Wednesday, June 10, 2009

WASANII WETU

SOME TIMES TUNAKULA NEWS. KUTOKA KUSHOTO DJ MULL B, JOE MAKINI, MATONYA, POLICE MAN MEMBER, PROF JAY NA JAY MOO NDANI YA 88.1FM MWANZA TOUR YA SHANGWE ALBUM.